JINSI YA KUTUMIA TECNO FLASH TOOL KUFLASH SIMU

Nakukaribisha tena kwenye page ambapo leo naendelea na mfurulizo wa mada zinazokufundisha namna ya kuflash simu kwa kutumia software mbali mbali za simu na hii leo nitaongelea software ya inayoitwa tecno flash tool.

Kwa kuanza ni vyema uifahamu zaidi software hii kabla hatuajaanza kujifunza jinsi ya kuitumia

TECNO FLASH TOOL NI NINI?


Hii ni software ya kuflashia simu za mediatek chipset ,imetengenezwa na kampuni ya Mekail92, kulingana na jina lake watu wengi wanazani app hii inatumika kuflashia simu za tecno pekee la hasha nimetumia hii software kuflashi simu ya infnix hot 8 bila shida yeyote, kwa hivyo unaweza kuflashia simu zingine zenye chipset ya mediatek.

Hii software ni bure kabisa haiitaji kulipia kisasi chochote cha pesa kuitumia, unachotakiwa kufanya ni kuidownload tu na kuanza kuitumia pia haina mb nyingi kwahivyo unaweza kuidownload haraka.

Kitu muhimu kujua ni kwamba kuhusu hii software ni kwamba.

  • Hii software ni kwa simu za tecno na infinix tu Haziwezi kuflash simu zingine kama vile simu za samsung na nyinginezo( labda ziwe na chipset ya mediateck)
  • Hii software inaflash simu kwa kuondoa mfumo(android) uliomo na kuweka mwingine kama uliokuwemo.
Software hii imetengenezwa kwa ajili ya computer zinazotumia windows os.

Baada ya kufahamu vitu hivyo muhimu tuendelee na kipengele cha kinachofuaata ambapo tutaangalia vitu vinavyoitajika ili kuweza kukamilisha lengo la kuflashi simu

JINSI YA KUDOWNLOAD TECNO FLASH TOOL


Kitu cha kwanza ni kuipakuwa(kudownload) toleo la sasa la software ya tecno flash tool, sasa hapa chini nimekuwekea link ambayo itakusaidia kudownload toleo la sasa la hiyo software kwa urahisi zaidi. Bonyeza hapo chini kuidownload.


Baada ya kuidownload hii software, utakuta ipo kwenye faili lenye zipu( zip folder) kwa hivyo li unzip kisha fungua faili litakalotoka , ndani utakuta mafaili mengi sana bonyeza faili lenye kapicha ka kijani lililoandikwa SWD - after sales kama ilivyoonekana apo chini

Baada ya kubonyeza hapo software yako itafunguka. Ukisha fika hii hatua sasa unaweza kuanza atua za kuflashi simu

JINSI YA KUITUMIA SOFTWARE YA TECNO FLASH TOOL

Ili kuitumia software hii kuflashi mfumo wa simu ( rom) kwenye simu yeyoye inayotumia mediatek chipset  kuna vitu vya muhimu lazima uwe navyokaribu. Hapo chini nimeorodhesha vitu vyote ambavyo unatakiwa kuwa navyo ili kukamilisha hili swala.

MAHITAJI YOTE

  • Computer
  • Waya wa usb ( usb cable) 
  • Lazima uwe umeinstall MTK VCOM driver
  • Simu unayotaka kuiflash lazima iwe inatumia chipset za mediatek (unaweza kuangalia mtandaoni kujua )
  • Unashuliwa uwe umechaji simu angalau asilia 50 (sio lazima sana ila akikisha sio chini ya ailimia kumi ili isije kuzima sababu ya chaji huku haijamaliza kuflash)
  • Faili la mfumo wa simu husika (firmware) hakikisha ni modeli ile ile ya hiyo simu (kuwa makini kuangalia isitofautiane hata namba wala herufi)

Kama hivyo vitu umevikamilisha anza kuflashi simu kwa kufuata hatua hizi

  1. Nenda kwenye software ya tecno flash tool ulipoi extract fungua kisha bonyeza SWD after sales kufungua hiyo software ikifunguka utakuta muonekano kama huu


2. Bonyeza kialama cha gia, kisha bonyeza kialama cha faili, hapo tafuta sehemu ulipohidadhifaili uliloweka faili la mfumo (firmware) unalotaka kuflash kisha lifungue kisha tafuta faili lililoandikwa Scatter.txt ,kisha libonyeze bonyeza confirm.


3. Baada ya hapo bonyeza alama ya kuplay ya kijani (kuanzisha), baada ya hapo zima simu yako chukua waya wa usb kisha chomeka kwenye computer na kisha kwenye simu yako, itaflash simu yako kikamilifu.


Asante kwa kufuatilia nakala hii andika maoni yako hapo chini kuhusu nakala hii.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post