JINSI YA KUBADILI ANDROID YA SIMU YEYOTE.

 Simu za android zina uwanja mkubwa sana wa kuzibadili kadri unavyotaka wewe lakini cha kushangaza bado watu wengi awafahamu ni kwa upana gani unaweza kubadili mfumo wa android wa simu yako.

 Sasa kama haukufahamu kabla leo nikujuze kuwa unaweza kuondoa mfumo yani android ya simu yako na kuibadili kuweka nyingine hapa simaanishi kuflash simu kama tulivyozoea hapa namaanisha kuondoa mfano android 9 kwenda android 10 au 11 au 12 kulingana na utakavyotaka wewe. Nimekuwa nikifanya hivyo kwa muda sasa leo nikeona ni vizuri kushare hiki kitu na wengine Wakifahamu kiundani zaid.

KWANINI UNAHITAJI KUBADILI ANDROID YA SIMU YAKO?

Kuna majibu mengi sana , binafsi nakumbuka nilikuwa nachoshwa sana na mfumo uliopo kwenye simu yangu kiasi ambacho ninaanza kutafuta theme mbalimbali lakini hazikuwa zinasidia kwasababu zilikuwa zinakaa juu ya huohuo mfumo wa android uliopo na watu wengi wanasumbuliwa na hiki kitu. Sasa hapa chini nimeweka sababu mbali mbali ambazo zimetatuliwa na kuweka mfumo mwingine kwenye simu

1. Kuondoa matangazo sumbufu

Nitachukulia mfano simu za tecno na infinix na nyinginezo kama oppo na xiaomi ambazo utaona matangazo mbali mbali yanajitokeza kwenye applications na zingine ni applications ambazo hauja zidownload ila zinakuja pia kuna zile ambazo zinakuja na simu na hauzitumii wala huwezi kuzifuta maarufu kwa kiingerez  kama bloatware, hivi vitu minaudhi sana kwenye simu na vinawekwa na makampuni ya simu kama infinix na tecno kwa sababu wanalipwa kufanya hivyo.

2. Kuondoa mifumo inayodhoofisha simu

Watu wengi wanalalamika kuhusu simu kuwa nzito au kugandaganda sana na wakati mwingine kufanya kitu kwa kuchukuwa muda mrefu sana, sababu kubwa huwa ni mifumo ya makampuni mfano kwa tecno (hiOS) na kwa infinix (xOS) , tukumbuke android ya simu inatengenezwa na google. Lakini makampuni ya simu yanaongeza kamfumo kadogo ambako kanakuwa juu ya original android mifumo hizi hutumika kuzitambulisha kampuni husika na zinatoa nafasi ya kampuni kuiweka android ya simu namna wanavyotaka ili kutofautiana na makampuni mengine , hiki kitu kinayapa makampuni  upenyo wa kuweka matangazo kwa kulipwa pia kuzuia baadhi ya vitu wanavyoona haviwapi wao faida, ukibadilisha mfumo wa simu hivi vyote vinaondoka unabaki na original Android kama ya simu za google pixel hambazo hupendwa sana na watu kutokana na mfumo uliomo pia simu itabaki nyepesi sana.

3. Kubolesha animation na uharaka wa simu( muonekano wakati ukifungua mafaili)

Kila Android mpya inapotoka huwa imeboreshwa zaidi ya iliyopita na kwenye kuboresha google wanaangalia sana vitu viwili 

  • Muonekano
  • Wepesi wa mfumo wa simu

Hapa kwenye muonekano tunaweza kuona vile mifumo hutofautiana kwa kubadilishiwa muonekano, kwa hivyo kama umechoshwa  na muonekano uliopo kwenye simu yako hautajutia kubadilisha android ya simu yako 

Kuhusu wepesi google wanajitahidi kufikia ule wa simu za iphone ambazo zenyewe husaidiwa na hardware pia. Google inahakikisha android mpya inaweza kupaform vizuri zaidi ya zilizopita .

4. Vitu vipya vinavyoongezwa 

Kadri teknolojia inavyokua vitu vipya vinazidi kugunduliwa hii ni sambamba na mifumo ya simu ambapo kila mwaka unatolewa mwingine ,ni wazi kuwa mfumo mpya hauwezi kuwa sawa na uliopita lazima kuna vitu vimeongezwa, sasa hauitaji kununua simu mpya ili kuenjoy hivyo vitu, unachotakiwa kufanya ni kubadilisha android ya simu yako.

5. Kupata mabolesho mapya ya software(software update)

Hapa kidogo ni sawa na pointi iliyopita, kwenye simu zetu huwa kuna kipengere cha software update ambacho kinatoa fursa ya kupata maborsho ya software hapo hapo kwenye simu yako, lakini kampuni zilizojikita huku hizi kama tecno na infinix hazito update za mfumo mzima wa android bali hutoa maboresho madogo madogo sana. Kwahivyo ukitaka kufurahia update hizi utazipata kwenye mfumo mpya utakao uweka.

6. Kubadili mpangilio kadri utakavyo (customization )

Hapa utaweza kubadili muonekano kadri utakavyo, kubadili staili ya icons, charge inavyoonekana, tarehe , kupata dark theme na vingine vingi utavigundua mbeleni ukiwa unatumia. Zipo sababu nyingi sana ambazo sijaziongelea wala siwezi kuzimaliza.


NINI MAANA YA CUSTOM ROM?

Custom rom ni mfumo wa android ulioboreshwa zaidi nikiwa na maana ya kwamba code za android zimetumia kutengeneza hizi custom rom lakini zimefanyiwa maboresho ili kuweza kutumiwa na simu nyingi. Simaanishi kuwa neno custom rom linamaanisha upande wa android tu, custom rom kama kaiOS na ios, lakini hapa tumejikita kwenye android  tu isitoshe custom rom nyingi utakazo kutananazo kuna chance kubwa zikawa ni za android. 

Kwahivyo ili uweze kubadilisha mfumo yani android ya simu yako ni lazima utumie hizi custom rom maana ikiwa sio custom rom haiwezi kuingiliana na simu yako.

NANI ANAETENGENEZA HIZI CUSTOM ROM?

Hapa Kama jina lenyewe custom rom , rom ndio mfumo(android yenyewe) na neno custom likiwa na maana ya kuboresha kadri utakavyo, basi kumbe custom rom ni android iliyoboreshwa kadri ya matakwa ya mtu. Hii ufanyika kwa sababu android ni mfumo ulio wazi yani data zilizotumika kutengeneza android zinapatikana kwa kila mtu na hii imeruhusiwa na google

Tukija kwenye swali letu "nani anaetengeneza hizi custom rom " jibu ni Kwamba mtu yeyote anaweza kutengeneza ili mradi tu awe na ujuzi huo , kwahivyo zipo custom rom nyingi lakini zimetengenezwa tofauti japo zote zimetokana na android lakini pia ukifuatilia utagundua zinatofautiana kidogo sana, custom rom utengenezwa kwa ajili ya aina tofuati tofauti za simu.

Baadhi ya custom rom maarufu ni kama :-

  • Aosp
  • Pixel experience 
  • Caos

JINSI YA KUBADILISHA ANDROID YA SIMU YEYOTE

Kama unataka kubadili android ya simu yako kuna vitu vingi vya kufahamu kabla ya yote ni lazima kujua kuhusu android gsi. Hii ni muhimu sana kuielewa 

ANDROID GENERIC SYSTEM IMAGE (GSI) NI NINI?

Hii ni aina ya custom rom ambayo ndio android yenyewe utakayo iflash kwenye simu yako, imefanyiwa maboresho ili kuweza kuflashiwa kwenye simu zote za android, ili useze luiflash hii gsi lazima simu yako iwe ina suport project treble.


NINI MAANA YA PROJECT TREBLE?


Google ilianzisha hii project kwa kutofautisha vendors ili kuwezesha makampuni kufanya malekebisho ya mfumo na kisha kupandisha kwenye simu(software update) kiurahisi zaidi.

Simu zinazo suport hii opareaheni zina itwa project treble devices, na ni zile zenye kuanzia android 8.1 na kuendelea kwahivyo kama simu yako inaandroid kwanzia 8.1 basi inasuport hii project treble na unaweza kuibadilishia android na kuweka android ya toleo la sasa lolote lile au kuweka la zamani kama utataka.

NITAJUAJE KAMA SIMU YANGU INASUPORT PROJECT TREBLE?

Ni rahisi kufahamu cha kufanya ni download application inayoitwa treble info kwenye play store( yenye picha ya rangi ya kijani ) zipo application nyingi lakini hii hutoa taarifa nyingi zaidi za muhimu. Kisha ifungue, utakuta muonekano kama huu hapa chini


Maelezo muhimu kabisa yanapatikana hapo mwanzoni kwenye neno required image ambapo kwenye hiyo picha imeandikwa your device needs an image file named ...... Haya maelezo yana maanisha simu inasuport project treble inahita gsi ya aina hiyo kuwekwa.

Baada ya kufahamu kuwa simu yako inasuport project treble unaweza kuanza hatua za kubadilisha android ya simu yako 

Hatua za kubadilisha android ya simu yako

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post