Kuna wakati mtu unakuwa umesahau neno la siri la simu yako , Katika hali hii utajiuliza je kuna njia yeyote rahisi na ya haraka inayoweza kufungua simu yako? Njia zipo lakini sio rahisi sana japo ni za haraka ila zinakuja na hasara zake ambazo ni kupoteza data zako zote ulizokuwa umezihifadhi kwenye simu kwa sababu njia hizi zitafuta kila kitu kilichopo kwenye simu yako.
Muhimu: Kama umesahau (haufaamu) gmail iliyopo kwenye hiyo simu ni bora usitumie hii njia kwa sababu ukishafuta kila kitu simu itaitaji uweke ile ile gmail ya kwanza ili kuendelea kuitumia sasa kama hauikumbuki itakutaka uiflash.
Nitakufunza njia rahisi kuliko zote ya kuformat simu yako. Pia unaweza kuta data za kwenye simu yako zimefutwa zote na mtu mwingine ukabaki unashangaa ukiamini akuna anaejua neno la siri ulioweka na wengine huenda mbali na kusema simu imejifuta la hasha simu ni computer inategemea mtumiajia aielekeze nini cha kufanya ndipo ifanye.
Hapa nitakufunza njia hizo rahisi kuliko zote ya kuformat simu yako. Pia mtu anaweza kutia njia hizi kufuta kila kitu kwenye simu yako hata kama hajui neno la siri kwahivyo kuta data za kwenye simu yako zimefutwa zote na mtu mwingine itakusaidia kujua ili usikabaki unashangaa ukiamini akuna anaejua neno la siri ulioweka na wengine huenda mbali na kusema simu imejifuta la hasha simu ni computer inategemea mtumiajia aielekeze nini cha kufanya ndipo ifanye.
Sababu za kuhitaji kuformat simu ni kama zifuatazo
- Kutaka kubadili neno la siri Baada ya kusahau neno siri lililopo au pateni (password) iliyopo kwenye simu
- Kuitaji kufuta data za simu kama vile picha na mafaili na kila kitu ulichowahi kuweka
Kabla sijaanza unatakiwa kukumbuka kuwa baadhi ya simu zinaweza kupishana na maelezo nitakayo toa hapa sababu baadhi ya simu hutofautiana mfano baadi ya simu zenye batani mbele chini ya kioo kama baadhi ya samsung na infinix note 7
Lakini maelekezo haya yataendana na simu za aina nyingi. Maelekezo yenyewe ni kama ifuatavyo......
Fuata hatua zifuatazo
1.bonyeza batani ya kuongezea sauti na ya kuwashia kwa pamoja kwa muda mlefu
Haijalishi simu itakuwa imewashwa au imezimwa , kama imewashwa bonyeza usiachie mpaka simu izime kisha iwake tena(ukishaona imewaka tu achia batani)
2. Ikishawaka itakuletea menu inayoitwa recovery mode hapo utakuta machaguo mbalimbali(sio simu zote zitakupeleka moja kwa moja kwenye machaguo).
Kama simu haijakupeleka moja kwa moja utakutana na neno no command, au fastboot au picha kama hii hapa chini.
Mfano mzuri ni simu ya infinix hot 8 , ukifika hapo bonyeza batani ya kuwashia bila kuiachia kisha bonyeza batani ya kuongezea sauti kwa haraka itakupeleka moja kwa moja kwenye machaguo ambayo yanaonekana kama hapo chini..
3. Tumia batani za kuongezea na kupunguzia sauti kuchagua wipe data/ factory reset kisha bonyeza batani ya kuwashia mara moja kuselect
Mpaka hapo simu itafuta kila kitu kisha itazima utatakiwa kuiwasha ili kuanza kuiseti upya.
NJIA RAHISI YA KUHIFADHI ZISIFUTIKE PALE SIMU INAPO KUWA IMEFLASHIWA
kwenye simu zetu kuna kumbukumbu nyingi sana za muhimu na ambazo uhitaji kuzipoteza pale unapopoteza , au kuflash simu yako. Zipo njia nyingi za kulinda data zako na hizi hapa chini ndio bora zaidi ninazopendekeza.
1. TUMIA AKAUNTI YAKO YA GOOGLE
Njia hii ndio pendekezo la kwanza Google inamiliki application nyingi za muhimu ambazo unazitumi marakwamara kama vile google photo, Google drive,google docs, messages, contacts na nyingine nyingi
Karibu hizi zote zimeunganisha na akaunti ya google pia zimeungwa kwenye hifadhi(storage) ya online inayojulikana kwahivyo unaweza kusave namba za simu, picha na nyaraka muhimu huko hapa hutawahi kupoteza hizo data , cha kuzingatia ni kuhakikisha hausaha gmail na neno lake la siri.



